Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi Mwanahamisi Munkunda leo Oktoba 22, 2023 ameungana na viongozi wa Chama na serikali Mkoani Mtwara kupokea Meli Kubwa yenye makasha zaidi ya 225 katika bandari ya Mtwara yatakayotumika kusafirisha Korosho kuelekea Nchi mbalimbali duniani.
Mkuu wa huyo wa Wilaya ya Mtwara Bi Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa ujio wa meli hiyo ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Wakati wa ziara yake Mkoani Mtwara ambapo aliuagiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha unaanza kuitumia bandari yake kusafirisha korosho Ili kupanua wigo wa soko la zao hilo.
Aidha Mhe Munkunda ametoa wito kwa wadau mbalimbali Mkoani Mtwara wakiwemo wafanyabiashara, wasafirishaji, wakulima, watoa huduma pamoja na wadau wote wanaoguswa na mnyororo wa thamani katika suala zima la Kilimo na usafirishaji wa Korosho kupitia bandari ya Mtwara kuchangamkia fursa hiyo Ili waweza kujikwamua kiuchumi.
" Ndugu viongozi mliopo hapa pamoja na Wanahabari, bila shaka wote mmeshuhudia mwisho ni mwa wiki tunayoimaliza Leo tulizindua mnada wa kwanza wa Korosho ambapo mpaka sasa tumeuza tani elfu 20" alisema Mhe Mwanahamisi Mnkunda.
" Hivyo ni matumaini yangu kuwa ujio wa meli hii utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wanamtwara wakiwemo mama ntilie, boda boda, bajaji, wamiliki wa Nyumba za kulala wageni halikadhalika wakulima na wanunuzi wa korosho kwa ujumla ninawaomba mchangamkie fursa" akisisitiza Mhe Munkunda.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe Munkunda ameuagiza uongozi wa Bandari ya Mtwara kujiweka Mkakati wa kuwavutia wamiliki wa meli Kutoka maeneo mbalimbali duniani wasafirishe mzigo wa Korosho kupitia bandari hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Mtwara Frednand Nyathi amemhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa tayari wamejipanga kuhakikisha mzigo wote wa Korosho utakaosafirishwa kupitia bandari hiyo unawafikia wateja kwa Wakati na kuongeza kuwa kutokana na uwepo wa miundombinu ya kisasa iliyopo kazi hiyo itatekelezwa kwa ufanisi.
Baadae mwezi ujao bandari ya Mtwara inatarajia kupokea zaidi ya meli 7 Kutoka Nchi mbalimbali zitakazofika kuchukua shehena ya Korosho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.