Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo amepokea Meli ya MV (Yasemin) Kutoka Nchi za Kiarabu. Meli hiyo Imetia nanga Bandari ya Mtwara huku Ikiwa Imebeba Shehena ya Salfa ya unga tani Elfu 2850. Mhe. Gaguti ametoa agizo la utekelezaji kwa mamlaka husika kusambaza Salpha hiyo kwa haraka.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu wa Chama Mkoa Mkoa wa Mtwara Alhaji. Saad Kusilawe na Mhe. Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.
Pichani; Mhe. Brig. Jen. Marco Gaguti akiongea na waandishi wa Habari leo wakati wa mapokezi ya meli MV Yasemin.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.