Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema watumishi wanaojitolea katika Sekta ya afya wanatakiwa kupewa kipaumbele. Dkt. Grace ameyasema hayo leo tarehe 09 Septemba 2025, alipokuwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa Sekta hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara baada ya kupokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa, CPA. Bahati Geuzye.
Lengo la ziara ya Dkt. Magembe ni kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya, Changamoto zilizopo kwenye Sekta hiyo, pamoja na kuzungumza na wataalamu na Watumishi wa afya ili kujadili mambo mbalimbali hasa yahusuyo maadili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.