Kikao cha PHC (Primary Health Care) kimefanyika mkoani Mtwara kwa lengo la kuhimizana na kupanga mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya Mapafu ( COVID -19). Kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa boma Mkoa na kimeongoza na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brig. Gen. Marco Elisha Gaguti na kuhudhuriwa na Katibu Tawala mkoa bwana Mohamed A Malela, waheshimiwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, waganga wakuu wa halmashauri, viongozi wa dini, wazee maarufu na wanahabari
Wengine ni timu ya usimamizi wa huduma za afya mkoa (RHMT), wakuu wa seksheni na vitengo kutoka sekretarieti ya mkoa Mtwara, wakuu wa taasisi zaambazo ni TMDA, MSD, NHIF, Hospitali ya rufaa ya Ndanda, na mameneja wa bandanri na kiwanja cha ndege Mtwara.
Katika kikao hiki, RMO aliwasilisha mada ya mwenendo wa ugonjwa wa CORONA nchini Tanzania na kueleza malengo ya nchi katika kupambana na COVID-19 yanayotolewa kupitia Wizara ya Afya.
Pichani; Wakati wa kikao cha PHC, RMO akiwasilisha mada ya mwenendo wa ugonjwa wa CORONA nchini kwenye Ukumbi wa Boma uliopo Ofisi ya Mkuu wa MKoa Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.