Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ashiriki maazimisho ya miaka 20 ya Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mashujaa.
Mkurugenzi wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kanda ya kusini, Bi. Rukia Semwaiko ameeleza wanufaika wa mkopo huo hupewa miaka miwili baada ya kumaliza chuo ili waanze kurejesha.
Bi Semwaiko aliongeza kwa kusema wapo wanufaika wa mkopo huo wa elimu ambao ni waaminifu hurejesha bila shuruti lakini kuna ambao bodi huwafuatilia kwa waajiri wao ili waweze kurejesha hivyo ametoa rai kwa wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu kuresha ili wengine waweze kukopeshwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.