Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ametoa rai kwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara kugawa misaada kwa wanachi walioathiriwa na mvua kwa kuzingatia utaratibu mzuri.
Ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 13 Machi 2025 alipokuwa akikagua misaada iliyotolewa kwaajili ya walioathiriwa na mvua zilizonyesha mapema mwezi Februari.
“Misaada iliyoletwa na Serikali yetu pamoja na ile iliyotolewa na wadau ni vema sasa tuigawe kwa wananchi kwa utaratibu ambao ni mzuri bila kuwa na tatizo lolote.” Alieleza Kanali Sawala
Aidha, Kanali Sawala amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kusaidia waliopatwa maafa hayo huku akitoa rai kwa wananchi hao kuendelea kusaidiana katika hatua mbalimbali za maisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.