Baadhi ya mabango yaliyowasilishwa kwa Mheshimiwa Majaliwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Newala
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka watumishi wa Umma kote nchinI kuhakikisha wanawatumikia wananchi katika misingi ya haki na maadili ya kiutumishi. Amesema huo ndio utumishi wa umma unaosisitizwa na serikalini ya awamu ya Tano na kwamba yeyote atakayeshindwa kutekeleza hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko katika siku ya pili ya ziara ya Kikazi Mkoani Hapa ameyasema hayo leo katika kikao na Watumishi wa Halmashauri za Wilaya na Mji wa Newala kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amesema taratibu za serikali zinaeleweka ambapo kila mtumishi wa Umma ana sehemu yake ya utekelezaji wa majukumu yake ya kazi ikiwemo kuwahudumia wananchi. Inapotokea nidhamu ikakosekana, ushirikiano hupotea na hatimaye kupoteza ufanisi wa kazi.
Ameongeza kuwa Kila Mtumishi wa Umma anapaswa kuijua ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo inatekelezwa. Hilo litamsaidia Mtumishi kufahamu nini anachotakiwa kufanya kwani watanzania walikiamini chama cha Mapinduzi na kukipa nafasi ya kuongoza nchi, kwa maana hilo kila mtumishi bila kujali imani yake au itikadi yake kisiasa anapaswa kuhakikisha anashiriki katika kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Awali akiwasilisha taarifa ya Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Newala Mheshimiwa Aziza Mangosongo amesema Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Newala zimejipanga kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya kwa weledi. Amesema ziko changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu hayo lakini wamejipanga kupambana nazo. Amezitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na miundombnu chakavu ya utoaji wa huduma ikiwemo matatizo umeme, barabara na Maji.
Nakuhakikishai Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba wananchi wa Newala wako tayari kuhakikisha ilani ya Chama inatekelezwa kama Serikali ya awamu ya tano ilivyoelekeza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa yuko katika ziara ya siku tatu Mkoani Mtwara. Katika Siku hizo tatu ambazo zitakamilika kesho Februali 28, Mheshimiwa Majaliwa atapita Wilaya zote tamo za Mkoa wa Mtwara akifanya vikao na kukagua miradi mbalimbali ya Mendeleleo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.