Mkoa wa Mtwara umesheherekea siku ya kuzaliwa kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa taulo za kike 1500 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika manispaa ya Mtwara Mikindani.
Shughuli hiyo imeongozwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas Ahmed akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali pamoja na wadau wa maendeleo iliyofanyika katika viwanja wa mashujaa mjini hapa.
"Namshukuru kwa mengi hasa anavyolipambania taifa la Tanzania katika nyanja mbalimbali, na katika jitihada hizo sisi wanamtwara ni wanufaika na ndo maana tukaona tukutane ili tulipe fadhila kukata keki kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake." alisema Kanali Abbas.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.