Uzinduzi wa msimu wa Kilimo katika Mkoa wa Mtwara umefanyika rasmi leo tarehe 30 Desemba 2024 ikiwa ni ishara ya kuaza rasmi kwa kilimo na uzalishaji wa mazao mbalimbali katika mkoa wa Mtwara.
Uzinduzi huo umefanyika katika Kijiji cha Mpindimbi Wilaya ya Masasi na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Christopher Edward Magala aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala.
Akizungumza katika uzinduzi huo DC Magala amesema Mkoa wa Mtwara unaendelea na mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo ukiwepo ufuta,Mbaazi na Korosho.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kujishughulisha na kilimo cha aina mbalimbali, kutokana na mazingira mazuri ya kuwezesha kilimo ambayo yamewekwa na serikali ya awamu ya sita.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Uzalishaji ambaye pia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bi. Nanjiva Nzunda amesema kuwa hali ya chakula katika mkoa wa Mtwara imeendelea kuwa ya kuridhisha.
Pia ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa usambazaji wa pembejeo kwa wakulima ikiwemo mpango wa kutoa ruzuku ya mbolea na mbegu za mahindi zilizothibitishwa ubora kwa wakulima
"Tunamshukuru sana Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukipa kipaumbele kilimo ambacho kimeendelea kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara na kuzidi kuwaimarisha kiuchumi" amesema Bi. Nanjiva.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.