Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) ametembelea katika kituo cha afya Mkunwa kinachojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo hicho.
Akiongea mara baada ya ukaguzi Mhe. Waziri Mkuu amemuagiza Mganga mkuu wa Wilaya kusimamia ujenzi wa kituo hicho ili kikamilike kwa wakati kwani Serikali inataka kuona wananchi wakipata huduma za afya wakiwa katika maeneo yao.
Aidha amewatoa hofu wananchi wa kijiji cha Mkunwa na kuwataka watoe hofu juu ya changamoto ya watoa huduma za afya kwani Serikali iko katika hatua za mwisho za kutoa takribani ya watumishi 400 ambao watapangiwa vituo vipya vya afya ikiwemo kituo cha Mkunwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.