Ikiwa ni muendelezo wa ziara iliyoanza mwishoni wa wiki iliyopita, leo tarehe 05 Mei 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Kanali Patrick Sawala ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Akiwa wilayani Tandahimba Kanali Sawala ametembelea mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana shule ya Sekondari Mdimba, Mradi wa Maji Mivanga, Kituo cha Afya Kitama, Barabara pamoja na Bodaboda waliopata mkopo wa 10%.
Kanali Sawala ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kwa kuweza kujenga bweni la wavulana Shule ya Sekondari Mdimba lililogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 160.9 kwa kutumia mapato ya ndani kupitia mfuko wa Elimu ambapo wanafunzi wapatao 120 wanatarajiwa kulitumia pindi litakapokamilika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.