Watumishi na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi wametakiwa kumpa ushirikiano Mkurugenzi wa sasa, Ndg. Alphaxard M. Etanga kama walivyokuwa wakimpa Mkurugenzi aliyekuwepo kabla, Bi. Beatrice Mwinuka ambae amehamishiwa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 24 Februari 2025 na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala alipokuwa akikagua miradi ya shule za msingi (BOOST) na za sekondari (SEQUIP) katika Halmashauri hiyo.
“Mkurugenzi huyu nimemuona ni kiongozi anaependa matokeo chanya, tumtengenezee mazingira mazuri ya kufanya kazi kwani miradi yote inakayotekelezwa ni yetu wana Mtwara.” Alieleza Kanali Sawala
Kwa upande wake Ndg. Etanga alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa miradi yote iliyopokea fedha mwezi Juni 2024 itakamilika ifikapo Machi 30, 2025.
Miradi iliyotembelewa katika halmashauri hiyo ni Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Msikisi, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata Mlingula na Ujenzi wa Shule Mpya ya Kata ya Mwena.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.