Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amewapokea na madaktari Bingwa 63 wa Dkt. Samia ambao watapiga kambi kwa siku 7 kuanzia leo tarehe 2 mpaka 7 Juni 2025 katika Hospitali za Halmashauri zote 9 za mkoa wa Mtwara.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo CPA. Bahati ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali afya za wananchi wa Mtwara kwa kuajiri watoa huduma za afya 587 na sasa kwa miaka mitatu mfululizo mkoa umeendelea kupokea madaktari bingwa wa Samia huku akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za kibingwa.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na huduma za afya kwa watoto na watoto wachanga; huduma za afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake na ukunga; huduma za magonjwa ya ndani (shinikizo la damu, kisukari nk).
Huduma zingine zitakazotolewa ni upasuaji (mfumo wa mkojo), huduma za ganzi na usingizi, pamoja na huduma za kinywa na meno.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.