MTWARA HADI COMORO NJIA NYEUPE.
Chemba ya Biashara na Kilimo Tanzania (TCCIA) kwa kushirikiana na muwekezaji kutoka visiwa vya Comoro wakiongozwa na kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Mwanahamis Munkunda wamezindua meli ya abiria kutoka Comoro kuja Mtwara.
Meli hiyo imezinduliwa leo katika Bandari ya Mtwara mara baada ya kuwasili Bandari ya Mtwara ikitokea Comoro kuleta abiria wakiwemo watu ambao wanakuja kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Muhimbili na Hospitali ya rufaa kanda ya Kusini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mwanahamisi Munkunda ameishukuru TCCIA pamoja na muwekezaji kwa kuanzisha meli ya kusafirisha abiria akisema hatua hiyo itaongeza ukuaji wa utalii wa matibabu nchini pamoja na Biashara.
Amesema serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kwa muwekezaji ili kuhakikisha usafiri huo unakuwa endelevu.
Akizungumza katika uzinduzi wa meli hiyo ya kwanza ya abiria tangu kufanyika uboreshaji wa Bandari, Makamu wa Rais TCCIA Swallah Said Swallah amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 300 na mizigo mchanganyiko wa vyakula tani 150.
Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake mara mbili kwa mwezi ikileta abiria kutoka Comoro kuja Mtwara na kutoka Mtwara kwenda Comoro ikipeleka mazao ya biashara.
Swallah amewataka wafanyabiara wa Mtwara kuchangamkia fursa ya kupeleka bidhaa za biashara hususan vyakula pamoja na mazao yote yanayolimwa kwenye mikoa ya Lindi , Ruvuma na Mtwara.
Aprili 19, 2024.
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.