Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2024/2025 wafunguliwa leo tarehe 11 Oktoba 2024 ambapo bei ya juu shilingi 4,120/= wakati bei ya chini ni shilingi 4,035. Katika mnada huo jumla ya tani 3,857 zimeuzwa.Mnada huo wa kwanza umeendeshwa kielektroniki kupitia Soko la bidaa Tanzania (TMX) na kushuhudiwa na Mkuu na Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ambapo amesisitiza ubora wa zao la korosho ndio utafanya bei izidi kuwa nzuri.
Kanali Sawala amesisitiza kuwa korosho yote itasafirishwa kupitia bandari ya Mtwara.
Wakulima wa korosho wameonesha furaha yao na kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwapa ruzuku za pembejeo bure.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wadau hao wa korosho kujitokeza kujiandikisha kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za mtaa, zoezi ambalo limeanza leo tarehe 11 Oktoba na litamalizika tarehe 20 Oktoba 2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.