Mkoa wa Mtwara unatarajia kupanda miti isiyopungua milioni tano kwa kipindi cha mwaka 2020. Miti hiyo itapandwa kupitia watu binafsi, vikundi na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za serikali.
Hayo yamebainishwa leo na Afisa Misitu Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara, Ronald Panga katika maadhimisho ya siku ya upandaji miti Mkoani mtwara iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, amesema Miti inayotarajiwa kupandwa ni pamoja na miti ya mbao, mijengo, kuni, mapambo, matunda na miti ya kilimo hususani mikorosho, michungwa na miembe.
Amesema upandaji huo utawezesha mkoa kufikisha miti milioni 15.1 iliyopandwa tangu kampeni hiyo ilipopewa msukomo mwaka 2015.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewata viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha wanasimamia sheria ili kuhakikisha ukataji miti holela unazuiwa. Amesema kesi nyingi ikiwemo ukati miti kwa ajili ya mkaa unaweza kuzuiwa iwapo wadau wote watashikamana, wakaungana katika kusimamia sheria na taratibu zizlizowekwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.