Mikoa ya Mtwara na Lindi imeendelea na maandalizi ya maonesho ya Nanenane 2017 yanayotarajiwa kufanyika kitaifa viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mapema wiki hii na wakuu wa mikoa hiyo miwili, Mhe. Halima Dendego, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mheshimiwa Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kusainiwa na Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi, Elibariki Mafole wamewataka wadau wote kuendelea na maandalizi kwa maelezo kuwa taratibu zote za kuandaa zimekamilika.
Wakuu hao wameeleza kuwa Wizara ya Kilimo, MIfugo na Uvuvi kupitia barua yenye kumbukumbu namba 18/45/01/121 ya Februali 10, 2017 ilitoa ruhusa kwa mikoa hiyo kuandaa maonesho hayo kwa ushirikiano ikiwa ni mara ya nne mfululizo.
Aidha wamewataka Wakuu wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wafanya biashara, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wanahabari na wadau wote kuhakikisha wanashiriki katika kikao cha maandalizi kitakachofanyika Aprili 12 mwaka huu katika viwanja vya Ngongo ukumbi wa Naliendele saa 3 asubuhi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.