• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

Mtwara-Mikindani yatumia Mili.834.1 kutekeleza miradi ya maendeleo

Posted on: January 19th, 2018

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani. Beatrice Dominic


Na Jamadi Omari. 

Afisa Habari Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Katika kuhakikisha Manispaa Mtwara-Mikindani inaendelea kuboresha huduma za Jamii kwa Wananchi wake, imetoa na kutumia fedha kiasi cha shilingi milioni  834,074,361.79 kutoka katika mapato yake ya ndani kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Akizungumza Ofisini kwake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Betarice Dominic amesema kuwa fedha hizo zimetokana na mapato yatokanayo na kodi mbalimbali zinazolipwa na Wananchi na kwamba Manispaa imeona umuhimu wa kuzirudisha kwao ili kuimarisha miundombinu mbalimbali inayowagusa moja kwa moja.

Amesema kuwa Miradi iliyopelekewa fedha imegusa sekta mbalimbali zikiwemo sekta ya elimu, Utawala, Ufugaji na Uvuvi, Barabara, Afya pamoja na Kilimo. Aidha amewashukuru na kuwapongeza Wananchi  wa Manispaa kwa kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi na kuwataka kuwa na utamaduni huo ili kuijenga Manispaa iliyo bora.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Manispaa Ernest Mwongi amesema kuwa fedha zote zilizotolewa zimeshapelekwa kwenye Akaunti za miradi husika na kuna miradi mingine imeshatekelezwa na kukamilika, na miradi mingine  ipo kwenye hatua ya utekelezaji na kwamba  idara  ya mipango inahakikisha inaifuatilia kwa ukaribu miradi iliyobaki ili iweze kukamilika kwa wakati.

Ameitaja Miradi inayotekelezwa kulingana na fedha iliyotolewakuwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi  wa zahanati Mbawala chini, UKarabati wa Machinjio, Ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Mbae na Mtawanya, Ujenzi wa Vyoo Shule za  Msingi Mjimwema, Shangani na Mlimani.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Kalvati Miseti, Ununuzi wa pikipiki 5 kwa ajili ya watendaji wa Kata, Ununuzi wa gari la Mkurugenzi, Ujenzi wa Uzio  Ofisi kuu ya Manispaa, Ujenzi wa Shedi mwalo wa samaki Mirumba, Ununuzi wa gari la kufagia barabara pamoja na Ujenzi wa nyumba  za Wakuu wa Idara.

Fedha hizo vilevile zimeelekezwa katika Ujenzi wa Ofisi ya Kata Mtawanya na Tandika, Umaliziaji wa ujenzi Ofisi ya Kata Jangwani, Ujenzi wa choo soko la kiyangu, Ujenzi wa nyumba za walimu Namayanga, Ujenzi wa soko la Mitengo, Uandaaji na ununuzi wa miche ya Korosho, Ununuzi wa mbegu za Mtama, uwekaji wa nguzo na minyororo barabara ya TANU, Ujenzi wa vyumba vya madarasa 3 Shule ya Sekondari Mitengo na Mangamba, Pia Utengenezaji wa madawati na uwekaji wa Taa Stendi kuu ya mabasi.

Asha Mapesa mkazi wa Chuno amepongeza Manispaa kwa kazi wanayoifanya ya kuleta maendeleo na kuahidi kutoa ushirikiano kwenye kulinda rasilimali hizo kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Baada ya kufanya Mapitio ya bajeti 2017/2018 mwezi Desemba 2017, Manispaa Mtwara-Mikindani imepanga kukusanya bilioni 4,601,204,136 kutoka katika mapato yake ya ndani, Hadi Desemba 31,2017 Manispaa imekusanya bilioni 2,720,578,528 sawa na asilimia 59 ya bajeti iliyopangwa.



Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • CRDB KANDA YA KUSINI YAISHIKA MKONO MTWARA MAANDALIZI YA UMISETA TAIFA

    May 27, 2025
  • KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MIKOKO 6,000 YAPANDWA MTWARA.

    May 31, 2025
  • KAMATI YA LISHE MKOA WA MTWARA YAKUTANA

    May 30, 2025
  • MIRADI YA UJENZI ITOE AJIRA KWA WANANCHI” WAZIRI ULEGA

    May 27, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.