Katika kikao kilichokutanisha wadau wa zao la korosho siku ya jana tarehe 04/09/2024 kwa lengo la kufanya tathimini ya zao la korosho msimu uliopita na kujadili mipango kwa msimu wa 2024/2025, Afisa anaeshughulikia Uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara, Bi. Nanjiva Nzunda alieleza kuwa kwa mwaka huu lengo la Mkoa wa Mtwara ni kuzalisha korosho tani 210,000
Kwa msimu uliopita Mkoa wa Mtwara ulizalisha tani 180,544 ikiwa ni ongezeko la 82% ukilinganisha na mwaka 2022/2023 ambapo tani 99,266 zilizalishwa.
Bi. Nanjiva alieleza kuwa kwa msimu wa 2023/2024 Bandari ya Mtwara ilisafirisha zaidi ya tani laki mbili kwenda nchi za India na Vietnam kutoka katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Aliendelea kuongeza kwa kusema tani 7,971 zilisafirishwa kwa njia ya barabara kuelekea Mkuranga, Mombasa-Kenya pamoja na Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya korosho, Bw. Francis Alfred ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa na wadau wote wa korosho kwa kuendelea kusimamia vema zao la korosho huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani zao hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.