Washiriki wa UMISETA mkoa wa Mtwara wakiingia katika eneo la uzinduzi
Mashindano ya UMISETA mkoa wa Mtwara yamezinduliwa jana katika uwanja wa chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida kilichoko mjini Mtwara. Jumla ya wanafunzi 301 watashindana katika michezo mbalimbali ili kuwapata 70 watakaopeperusha bendera ya Mtwara katika mashindano ya kitaifa yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mjini Mwanza.
Akizungumzia mashindano Hayo, Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Fatuma Kilimia amesema mandalizi yote yako sawa na kwamba wanatarajia kuwapata washiriki bora ambao watawawakilisha vema katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Mwanza kuanzia Juni 6 hadi 16 mwa ka huu.
Kwa upande wake Afisa Michezo Mkoa wa Mtwara Rodgers Bahati amesema wanamichezo wako katika ari na moyo wa ushindi na kwamba mkoa unamatumaini makubwa ya kuwapata washindani hodari. Amesema kaulimbiu ya ya Umiseta mwaka huu ni ‘Tuwekeze katika michezo kwa ustawi wa elimu na viwanda Tanzania’ na kwamba kudumisha michezo kutasaidia kuvipata viwanda ambavyo vitapunguza soko la nje la bidhaa za michezo na hivyo bidhaa nyingi kutengenezwa hapahapa nchini.
Aidha Jenipher Erasto mchezaji wa Volleybal anasema mashindano haya yatawafanya waonekana kimataifa na kwamba maandalizi waliyoyafanya kuanzia mashuleni yanatosha kuleta ushindi kwa mkoa wa Mtwara.
ili kutazama video ya tukio hilo Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.