Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitasita kuchukua hatua kwa atakaebanika kuwa na nia ya kuondoa amani ya muungano.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika leo tarehe 25 Aprili 2025.
“Muungano huu una faida nyingi, leo wananchi wa Mtwara wanaweza kufanya kazi, kuoa au kuolewa Zanzibar, kadhalika na Wazanzibari; tusiwape nafasi wanaotaka kutugawa.” Alieleza Mhe. Hemed
Aidha, Mhe. Hemed amewataka wananchi wa Mtwara kuendelea kujituma kufanyakazi kwa bidii ili kuzidi kudumisha uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Mhe. Hemed amewaomba wananchi wote wenye sifa za kupiga Kura, wajitokeze kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 hukuakiwasisitiza kumchagua kiongozi sahihi.
“Muungano wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa; Shiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.