Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye kuupokea Mwenge wa Uhuru Mei 17,2025.
Mwenge huo ambao utapokelewa Kijiji cha Lumesule Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara utakimbizwa na kukagua miradi mbalimbali iliyopo kwenye Halmashauri tisa zilizopo mkoani humo.
"Tarehe 17,2025 tutapokea Mwenge wa Uhuru ukiwa unatokea kwa wenzetu Ruvuma tutaupokelea wilaya ya Nanyumbu na utakimbizwa kwenye mkoa wetu kuanzia hiyo mei 17 hadi mei 25,2025 kwa halmshauri zote tisa kilasiku itakuwa halmashauri moja moja."Amesema Sawala
Hivyo Sawala amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuupokea Mwenge na kushiriki kwenye shughuli zote za ukimbizaji wa mwenge huo,miradi mbalimbali ya maendeleo,mikesha na kwenye kukabidhi mwenge mkoa wa Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.