Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango leo tarehe 02 Aprili 2025 ameongoza uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mkoa wa Pwani huku akisisitiza umuhimu wa kuwafichua wahujumu wa rasilimali za umma bila woga. Dkt. Mapango pia aliagiza viongozi wa mikoa kushirikiana na wakimbiza Mwenge kufanikisha utekelezaji wa miradi inayotarajiwa kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa alisema Mwenge wa Uhuru unahamasisha mshikamano na maendeleo.
Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2025 Ndg. Ismail Ussi tayari kukimbizwa katika mikoa 31 na halmashauri 195 ambapo mkoa wa Mtwara utapokea Mwenge huo tarehe 17 Mei 2025 na kuukimbiza katika Halmashauri zake 9 hadi tarehe 25 Mei 2025.
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru ya mwaka huu 2025 ni “Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.