Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 17 Mei 2025 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo ukiwa unawaka na kumeremeta tayari kwa kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo katika Halmashauri 9 za mkoa wa Mtwara.
“Mwenge wa Uhuru umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini, ulete upendo mahali penye chuki na heshima mahali palipojaa dharau.”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.