Mwenge wa Uhuru leo Agosti 28, 2021, umepokelewa Mkoani hapa, ambapo ukiwa katika Mkoa huo, Utapita katika Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara na kufanya shughuli za kuzindua, Kuweka Mawe ya Msingi na kukagua Miradi yenye thamani ya Shilingi bilion 11,100,249,345
Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Lindi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyoba, amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Mtwara utakimbizwa kwenye Wilaya zote 5 za Mkoa huo, kuanzia leo tarehe 28 Agosti hadi Septemba Mosi,2021.
"Mwenge wa Uhuru utapitia jumla ya miradi 42 yenye thamani ya (Bilioni kumi na moja, Milioni mia moja, Laki mbili arobaini na tisa elfu, Mia tatu arobaini na tano), amesema Kyoba na kuongeza kuwa,
katika Miradi hiyo Michango ya wananchi ni shilingi 1,105,813,300 sawa na asilimia 10%, Serikali kuu shilingi 7,014,109,149 sawa na asilimia 64, huku fedha za Wahisani ikiwa ni shilingi 1,925,467,895 sawa na asilimi 17.
Kwa upande mwingine Michango hiyo imezihusisha Wilaya zilizofanikiwa kuchangia shilingi 1,054,859,000 sawa na asilimia 9.
Taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaonesha, Mwenge wa Uhuru utaweka mawe ya Msingi miradi 8, kufungua miradi 5, kuzindua miradi 7 na kuona na kukagua miradi 22.
Kyoba amesema, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye umbali wa km 556 na Kiongozi wa mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Paul Mwambashi.
Mwenge wa Uhuru utahitimisha Mbio zake mkoani humo Septemba Mosi na Septemba 02 utakabidhiwa mkoani Ruvuma kwenye kijiji cha Sauti Moja.
Aidha baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Luteni Josephine Paul Mwambashi Kiongozi wa mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amezindua vitabu vya Sera ya TEHAMA Mkoa wa Mtwara.
Pichani: Kiongozi wa mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Paul Mwambashi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Masasi Kitabu cha Sera ya TEHAMA Mkoa mara baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.