Halmashauri ya Mji nanyamba imekabidhi madarasa 9 mapya ya shule za sekondari kwa Mkuu wa wilaya ya mtwara Mhe. Dunstan Kyobya yaliyojengwa katika mradi wa serikali wa kuhakikisha wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wanapata elimu bora. Madarasa hayo yamekabidhiwa na Mkurugenzi wa halmashauri Mji Nanyamba Ndg. Thomas Mwailafu baada ya ukaguzi uliofanywa katika shule ya sekondari Mtimbwilimbi, Mnyawi sekondari, pamoja na Dinyecha sekondari akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mtwara, viongozi wa vijiji pamoja na wanachi.
Akipokea madarasa hayo Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Kyobya amewashukuru viongozi na wananchi kwa kujitoa kwao kukamilisha ujenzi huo na kuwataka waendelee kuhamasishana katika kuwasajili watoto ili madarasa hayo yakatumiwe ipasavyo katika utoaji wa elimu.
Pia ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea wilaya ya Mtwara Bilioni 1 na milioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ambayo yote yameshajengwa na yako tayari kutumika. Mhe. Kyobya amewaomba wazazi wawe na utayari wa kuwaandikisha watoto na wakifuatilia maendeleo ya watoto wao ili kukomesha utoro.
Aidha amewataka wananchi waendelea kudumisha amani, kupinga ukatili wa kijinsia, kupinga vitendo vya ushoga kwa kushirikiana na viongozi wao ili kutengeneza jamii bora ya baadae
Makabidhiano ya madarasa hayo yamefanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Dinyesha katika halmashauri Mji Nanyamba.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.