Kufuatia athari zilizotokana na mvua zilizonyesha mapema mwezi Februari 2025 mkoani Mtwara, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo cha Uratibu na Maafa imewasilisha misaada ya kibinadamu katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara kwaajili ya kusaidia waathiriwa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo tarehe 09 Machi 2025, Bi. Consolatha Mbanga, Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu alianza kwa kupongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara pamoja ya ile ya Mkuu wa wilaya kwa namna walivyoratibu ukusanyaji wa misaada ya waathirika wa mvua hizo.
“Misaada tunayowasilisha hapa ni pamoja na Tani 21 za mahindi ambazo ni sawa na gunia 125, magodoro, mablanketi na chandarua 213, sahani, sabuni, mikeka, ndoo, madumu ya maji na pesa kiasi cha Shilingi 13,232,000/= ambazo zimewekwa kwenye akaunti ya Halmashauri ya Manispaa kwaajili ya kununua maharage.” Alieleza Bi. Consolatha
Kwa upande wake Mhe. Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa wilaya Mtwara amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa misaada hiyo.
“Baada ya maafa yale ya mvua tulikutana na wadau mbalimbali kwaajili ya kutushika mkono tuwasaidie wenzetu. Kipekee niwashukuru sana kwani misaada mliyotupatia leo itasaidia waliothiriwa na mvua pamoja na wenye uhitaji.” Alisema Mhe. Mwaipaya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.