Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Mikindani Mkoani Mtwara Abdul Masamba amepoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa baada ya radi kupiga katika moja ya darasa la shule hiyo asubuhi ya leo Machi 5, 2019. Akizungumzia tukio hilo Mwalimu Elizabeth Moses wa shule hiyo amesema tukio hilo lilitokea saa 4 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Amesema radi ilipiga mara ya kwanza, kisha baada ya dakika kama tano ikapiga tena, wakasikia kelele kutoka darasa la kidato cha tatu A. Walienda wakakuta wanafunzi wamelala chini. wakaanza kuwatoa nje na kuwawaisha zahanati ya Mikindani. Kwa bahati Mbaya mmoja akafariki kabla ya kufikishwa Hospitali.
“Tunashukuru kwa ushirikiano tulioupata kutoka kwa wananchi wa Mikindani, Madereva, Mwenyekiti wa Bodi, Ofisi ya Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. .” Amesema Mwalimu Elizabeth
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda ameshukuru hatua za haraka zilizochukuliwa na zahanati ya Mikindani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Ligula.
Hakuna kilichochelewa. Kila kitu tulikikuta mahali pake. Walipokelewa na wanaendelea kupata huduma vizuri. Amesema Mmanda.
Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula. Dkt. Lobikieki Kisambu amesema wamepokea Majeruhi 24. Wavulana 10 na wasichana 14 ambapo wawili wameruhusiwa kuondoka na wengine wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri
Video HII HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.