Rais Dkt. John Magufuli ameagiza zabuni ya ujenzi wa barabara kati ya Mnivata hadi Masasi mjini umbali wa takribani kilometa 150 itangazwe mara moja. Agizo hlo amelitoa leo Mjini Newala akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa. Utekelezaji wa agizo hilo utaifanya wilaya zote za mkoa wa Mtwara kuunganishwa kwa lami. ujenzi unaoendelea sasa ni kilometa 50 kutoka Mtwara hadi Mnivata umbali wa kilometa 50.
Akizungumzia uamuzi huo Mheshimiwa Magufuli amesema lengo la serikali ni kuhakikisha mkoa wa Mtwara unaunganishwa na nchi jirani ikiwemo Msumbiji na Malawi ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi hizo pamoja na mikoa yote ya kwenda mataifa mengine.
Amesisitiza kwamba ndiyo maana serikali iliamua kuwekeza katika upanuzi wa Bandari ya Mtwara pamoja na uwanja wa Ndege wa Mtwara lengo likiwa kuwezesha bidhaa na abiria wa ndani ya nje ya nchi kuifikia Mtwara kwa urahisi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amepongeza uamuzi huo na kusisitiza kuwa barabara hiyo ina umuuhimu mkubwa kwa uchumi wa Mtwara hasa kutokana na usafirishaji wa zao la korosho ambao unafanyika kupitia barabara hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.