Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 30, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema Mheshimiwa Rais atakuwa akitimiza ahadi yake aliyowaahidi wananchi wa Mkoa wa Mtwara Machi, 2017 wakati alipotembelea mkoani hapa.
Amesema Mheshimiwa Rais aliahidi kuja kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara inayotoka Mtwara mjini hadi kijiji cha Mnivata umbali wa kilometa hamsini.
Katika kikao hicho ambacho Mheshimiwa Byakanwa aliwaaalika wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumlaki Mheshimiwa Rais amesema Rais atatembelea wilaya zote za mkoa wa Mtwara, kukagua, kufungua na kuweka mawe ya Msingi kwenye miradi mbalimbali.
Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege Mtwara, mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata, ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin ambacho ni cha mtu binafsi, na Mradi wa uboreshaji wa miundombinu Chuo cha Ualimu Kitangali.
Miradi mingine ni ule wa ujenzi wa kituo cha afya Mbonde na mradi wa barabara ya Mangaka-Nakapanya-Tunduru na Mangaka-Mtambaswala.
Aidha, Mheshimiwa Rais atapata fursa ya kusalimia na kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.