Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala leo tarehe 31 Desemba 2024 amekabidhi msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 8 kwa vituo 6 vya watoto yatima na wenye uhitaji maalumu.
Vituo vilivyopatiwa msaada huo ni pamoja na; Mikindani Yatima foundation, EAGT Rahaleo, Upendo Rehabilitation Centre, Shule ya msingi Lukuledi maalumu, Shule ya msingi maalumu mji mpya na FPCT.
Kila kituo kimepatiwa madaftari pisi 80, kauntabuku pisi 192, kalamu, mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maji ya kunywa, juisi na mbuzi.
Kanali Sawala amewashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono wazo hilo la kuwagusa wahitaji.
Katika hatua nyingine, Kanali Sawala amewataka walezi wa watoto hao kuhakikisha wanawapeleka shule pindi shule zitakapofunguliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.