Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Gasper Byakanwa amewataka wakulima wa mkoa wa Mtwara waiamini na kuitumia huduma ya Tigo Korosho katika kupata malipo ya mauzo ya korosho. Amesema huduma hiyoni nzuri hasa katika kipindi hiki ambacho mauzo ya korosho yanafanyika.
Mheshimiwa Byakanwa ameyasema hayo leo mara baada ya kukutana na viongozi wa kampuni ya Tigo Kanda ya Kusini ofisini kwake. Amesema utaratibu wa sasa wa malipo ya korosho ni tofauti na miaka ya nyuma kwani sasa pesa zote zinalipwa kupitia huduma za fedha ikiwemo Benki na kampuni za simu badala ya utaratibu wa zamani wa kulipwa kwa viongozi wa Vyama vya Msingi.
Amesema tigo korosho itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa benki na kuharakaisha huduma kwa wananchi.
Ametoa shuklani za pekee kwa wadau mbalimbali wakiwemo Bodi ya Korosho. Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha, Vyama vya Ushirika na wadau wengine wote ambao kwa pamoja wamewezesha fursa ya kufikisha fedha za wakulima kwa urahisi zaidi.
Awali akitoa taarifa ya huduma za kampuni kupitia tigo Korosho, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini George Lugata amesema hadi sasa kampuni hiyo iliyoanzisha huduma hiyo msimu huu imesambaza jumla ya shilingi 330,343,529. Amesema kinachotakiwa ni mteja kujiandikisha katika mfumo wa tigo pesa na kuwasilisha vielelezo vyake kwa chama chake cha Msingi akiridhia kupata malipo yake kwa njia ya tigo korosho.
Amesema kupitia tigo Korosho mklulima analipwa fedha za mauzo ya korosho kwenye simu yake moja kwa moja bila kuhangaika kusafiri au kusubiri aletewe fedha yake.
Aidha, mteja wa tigo korosho anaweza kuhamisha fedha kiasi cha shilingi 200,000 Bila kukatwa makato yoyote.
Video yake hii HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.