Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti, amewataka wananchi katika Mkoa huo na maeneo ambayo Gesi imepita, kuendelea kuilinda Miundombinu ya Gesi ili iendelee kuwa na faida kwao wenyewe lakini Taifa kwa Ujumla.
Brigedia Gaguti amefikia adhma hiyo Mara baada ya ziara ya kutembelea maeneo ya vyanzo na uzalishaji wa gesi na Mitambo ya kuchakata Gesi asilia MSIMBATI - (M&P) MNAZIBAY na TPDC- MADIMBA
"Nimekuja hapa leo, lengo likiwa ni kupata uelewa wa jumla na kuona uendeshwaji wa Shughuli mbalimbali zinazoendelea ikiwa ni ziara yangu ya kwanza kwenye maeneo haya" Amesema Gaguti.
Brigedia Jenerali Gaguti pia amewapongeza TPDC na wadau wao kwa kazi nzuri ya uzalishaji wa Gesi ambayo inawezesha kuwepo kwa nishati ya Umeme wa uhakika kwa Mkoa wa Mtwara na Lindi pamoja na takribani asilimia 50 ya Umeme kwenye Mkoa wa Dar Es Salaam .
"Nitoe rai kwa wananchi wa Mtwara na maeneo yote ambayo Gesi inapita kuendelea kuitunza miundo mbinu ya Gesi kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla" amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa na kuwataka TPDC kuendelea kuwajengea uwezo watanzania ambao kwa sasa kwa asilimia kubwa ndiyo wanao ongoza Mitambo hiyo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ameendelea kuhamasisha wazawa kupenda kusomea vitu ambavyo Tanzania ina malighafi ya kutosha ikiwemo Gesi asilia na mengineyo ili waweze kuhimili kufanya kazi kwenye maeneo hayo.
Pichani; Mhe. Gaguti (Kulia) akipewa maelezo na Meneja wa Kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia cha Madimba Leonce Mrosso (Kushoto)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.