Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen. Marco Gaguti amewataka wananchi wanaofanya biashara Sabasaba na maeneo mengine kuhamisha bidhaa zao na kuhamia soko la chuno. Amesema kuwa tayari ofisi yake imeshatoa maelekezo ya kutaka biashara zote kuhamia soko la Chuno na kwamba itasimamia kuhakikisha wafanyabaishara hao wanahamia Sokoni hapo. Gaguti ametoa maagizo hayo leo Mei 31,2021 alipofanya ziara yake ya kwanza ya ukaguzi wa Soko la Chuno pamoja na kuongea na wafanyabiashara wa soko hilo.
Katika kuhakikisha soko hilo linaendelea kufanya kazi amewasisitiza wananchi wote wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutumia soko la Chuno kupata huduma mbalimbali badala ya kutumia masoko mengine. “Itakuwa ni dharau sana kwa Serikali imetuletea soko Zuri halafu hatutaki kulitumia ni dharau kwa watanzania pia kwa sababu fedha hizi ni kodi ya wananchi tulitumie soko hili vizuri”. Amesema Gaguti
Wakati huo huo Gaguti ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi Bilioni 5.3 za ujenzi wa soko la hilo na kuwataka wafanyabaishara kutoa huduma iliyo bora na kuuza bidhaa bora ili kuwapata wateja badala ya kuamini imani za kishirikina. Aidha amewaahidi kuwapa ushirikiano wajasiriamali wadogo waliopo kwenye Mkoa wake ili waweze kufanya biashara kwenye mazingira mazuri na kuiongezea kipato. Hii ni ziara yake ya kwanza kufanya ndani ya Mkoa wa Mtwara tangu alipoteuliwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mei 15 Mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.