Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 08 Februari 2025 amemkabidhi mkandarasi mradi wa ujenzi wa visima vitano vya umwagiliaji kwa mkoa wa Mtwara.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika kata ya Kitere, kijiji cha Lolido. Kanali Sawala ameeleza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita tangu mkandarasi akabidhiwe ambapo unatarajiwa kukamilika 21 Agosti 2025 ukitarajiwa kunufaisha wakulima 625 wa mbogamboga na mpunga.
“Mkoa wa Mtwara vitachimbwa visima vitano, kata hii ya Kitere mtapata visima viwili, kimoja ni cha umwagiliaji wa bustani wa mbogamboga na kingine kitatumika kuongeza maji katika skimu ya umwagiliaji.” Alieleza Kanali Sawala.
Aidha, Kanali Sawala amemuagiza mkandarasi huyo kukamilisha mradi ndani ya muda huku akiwataka wananchi kuvitunza visima hivyo pindi vitakapokamilika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.