Mheshimiwa Mmanda akila kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mbele ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Halima Dendego (hayupo Pichani), Januari 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amethibitisha kutokea kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda aliyefariki usiku wa kumukia leo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mtwara, Ligula alikokuwa akipatiwa matibabu.
“Jumamosi jioni alilazwa kwenye hospitali yetu ya rufaa ya mkoa Ligula. Jana jioni niliongea naye akanieleza kwamba anaendelea vizuri lakini jioni hali yake ilibadilika”.
Mheshimiwa Byakanwa amesema mazishi ya Mhe. Mmanda yatafanyika mjini Mtwara na kuhudhuriwa na watu wasiozidi kumi yakiongozwa na serikali.
“Kama mnavyojuwa tuko katika kipindi kigumu sana cha ugonjwa wa CORONA. Tuna makatatazo mbalimbali ya kuzuia mikusanyiko na misongamano ya aina yoyote. Kutokana na utaratibu huo nishukuru familia ya marehemu Pamoja na ndugu tumekubaliana kwamba sisi serikali ndiyo tutakaosimamia mazishi yake na hatutakuwa na kusafirisha mwili. Mazishi yatafanyika hapa Mtwara.”
Byakanwa ametoa pole kwa wanamtwara, wanaCCM, na watumishi wote. Amesema Mheshimiwa Mmanda alikuwa mchapakazi shupavu ambaye alikuwa amejitoa muda wake mwingi katika kuitumikia nchi. Mwenyezi Mungu amempenda Zaidi tunapaswa kuendelea kumuombea kwa mwenyezi Mungu. Amesema Byakanwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.