Mkuuwa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewahimiza wananchi wa wilaya yaMasasi kupanda zao la mhogo ili waweze kujiongezea chakula na kipato kutokana nazao hilo kuwa na soko zuri.
Hayo ameyasema Leo aliposhiriki zoezi la kupanda mihogo katika shamba la mfano kijijini Chisegu Wilayani Masasi mkoani Mtwara.
MheshimiwaByakanwa ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Oktoba 26 mwaka jana amekuwa na kampeini kubwa ya kuhamasisha kilimo cha zao hilo ambalo ni zao kuu la chakula mkoani hapa. Lengo la hamasa hiyo ni kuepukana na njaa, pia njia mbadala ya kujiongezea kipato.
Lichaya hamasa ya zao la mhogo Mheshimiwa Byakanwa amekuwa akiwasisitiza wananchi kulima zao la Korosho kama zao la biashara ambapo ameitaka Bodi ya Korosho pamoja na wadau wote wa kilimo kuhakikisha wanajiandaa ipasavyo kuondoa changamoto zote za uzalishaji wa mazao mkoani Mtwara.
Aidha amewataka vijana kujiunga katika vikundi vya kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo mihogo kwani mbegu za kisasa zinapatikana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.