Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 09 Septemba 2025 amefanya kikao na wananchi wa kijiji cha Nanganga wilaya ya Masasi kwa lengo la kusikiliza na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
Kanali Sawala ametumia kikao hiko pia kuwakumbusha na kuwasisitiza wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao ili kuwatengenezea kesho nzuri huku akiwataka kushirikiana vema na kamati ya elimu kwa masuala mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.