Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ameishukuru Jumuiya ya maridhiano na viongozi wa dini kwa namna wanavyoshirikiana vema na serikali katika kuhakikisha amani na utulivu vinadumu mkoa wa Mtwara.
Kanali Sawala ametoa shukrani hizo mapema leo tarehe 31 Desemba 2024 alipokutana na viongozi wa dini pamoja na jumuiya ya maridhiano mkoa wa Mtwara.
“Wote mnafahamu uchumi una mahusiano na usalama, naomba mkawasisitize waumini wenu walinde amani. Sisi serikali tutaendelea kusimamia haki kwani nayo ina uhusiano na usalama. Mkiona kuna changamoto mahali msisite kutuambia.” Alieleza Kanali Sawala
Aidha, Kanali Sawala amewashukuru viongozi hao wa dini kwa Dua na Sala zao ambazo zimesaidia mkoa kuvuna mazao kwa wingi, kuuza kwa bei nzuri na hata kuwa na akiba ya chakula.
“Elimu haina mbadala ili tuwe na taifa lenye maendeleleo, niwaombe viongozi wangu muwahamishe wazazi ambao ni waumini wenu wapeleke watoto shule pindi Shule zikifunguliwa.“
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.