Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala mapema leo tarehe 20/12/2024 amefungua na kuongoza kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Mtwara ambacho kimelenga kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya barabara mkoani Mtwara pamoja na Mpango na Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa TANROADS na TARURA.
Meneja wa TARURA mkoa wa Mtwara, Mhandisi Zuena Mvungi ameeeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 mkoa wa Mtwara umeidhinishiwa jumla ya Shilingi Bilioni 23.53 ambazo zitatumika kujenga barabara za lami zenye urefu wa km 21.37, barabara za kiwango cha changarawe kwa urefu wa km 125.75. Fedha hizo pia zitajenga makalvati 12 mapya makubwa (box culvert), makalvati madogo 15 ya 900mm, pia kujenga mifereji m 7,110.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Malaalum), Mhe. George Huruma Mkuchika ameeleza kuwa “Katika miji iliyopangwa vizuri na waingereza ni Mtwara na Tanga. Mtwara ukiwa unakuja kwa ndege unauona barabara zilivyonyooka, huu mji umepangwa kisasa, ila sasa usiku kuna giza, naomba barabara ziwekwe taa.”
Kanali Sawala amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote 9 za mkoa wa Mtwara kushirikiana vema na TANROAD pamoja na TARURA ili kufikisha maendeleo kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.