Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara, Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala ametembelea maeneo mbalimbali kuona athari zilizotokana na mvua hizo ili kuzipatia ufumbuzi.
Mamalaka ya hali ya hewa nchini Tanzania (TMA) ilitoa angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Lindi na Mtwara, Ruvuma na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
“Mvua ni neema lakini ikizidi inakuwa balaa, tunaona mvua hizi zimeharibu miundombinu yetu na kuleta madhara kwa wananchi; nimezielekeza mamlaka zinazohusika kuhakikisha wanatafuta suluhusho la muda mfupi na la kudumu kwa miundombinu yetu.” Alieleza Kanali Sawala
Aidha, ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa wahanga wote wa mvua hizo.
“Wataalamu wanafanya tathmini kujua mahitaji halisi yanayohitajika kama msaada kwa wananchi ili tuje kuwashika mkono wa pole.” Aliongeza Kanali Sawala.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.