Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ameipongeza Halmashauri ya Mji Masasi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Ametoa pongezi hizo leo tarehe 24 Februari 2025 alipotembelea na kukagua Ujenzi wa Shule mpya ya sekondari Matawale unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 560.55 ambao umefikia 95% ya utekelezaji.
“Kuleta fedha ni kitu kimoja, kuzisimamia ni kitu kingine. Niwashukuru na kuwapongeza Mhe. Mkuu wa wilaya, Mukurugenzi na timu yote kwa kusimamia vema na matokeo yanaonekana.” Alieleza Kanali Sawala
Aidha, Kanali Sawala ametoa wito kwa wazazi kushirikiana vema na walimu pamoja na uongozi wa shule kuhakikisha wanafunzi wanasoma ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata chakula cha mchana wawapo shuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.