Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya Sekondari Kilimanihewa uwe umekamilika.
Kanali Sawala ametoa agizo hilo leo tarehe 24 Februari 2025 kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika serikali za mitaa hususan miradi ya shule za msingi (BOOST) na sekondari (SEQUIP).
“Shule hii ilipaswa kuwa imekamilika tangu Januari 30,2025, taarifa yenu hapa inasema mtakamilisha mwisho wa mwezi huu lakini zimesalia siku nne tu na kwa hatua iliyobaki sioni mkikamilisha ndani ya huo muda. Sasa, Mkurugenzi mpaka kufikia tarehe 15 Machi 2025 ujenzi uwe umekamilika.” Alisema Kanali Sawala.
Ujenzi wa Shule hiyo yenye gharama ya zaidi ya Milioni 560.55 uliofikia 90% unatarajiwa kupunguza changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu hivyo utaondoa utoro na kuongeza ari ya wanafunzi kuhudhuria shuleni na kuinua kiwango cha ufaulu.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Mtwara amechangia kiasi cha shilingi Milioni moja kwaajili ya umaliziaji wa shule ya msingi Mwambani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.