• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

RC SAWALA AWATAKA VIONGOZI KUFUATILIA MIRADI KWA UKARIBU KUEPUKA MAKOSA

Posted on: December 23rd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ametoa rai kwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mikindani kushirikiana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia mafundi kwa ukaribu ili kuhakikisha miradi inatekelezeka kwa viwango vizuri.

Kanali Sawala ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 23 Desemba 2024 alipokuwa akitembelea miradi ya maendeleo.

“Injinia, Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine wote, niwaombe msimamie kwa ukaribu shughuli za ujenzi ili kuepuka gharama za ziada zitakazoweza kujitokeza ikiwa fundi amefanya kosa litakalogharimu kuvunja na kujenga tena.” Alieleza Kanali Sawala

Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa Mkoa ni pamoja na ujenzi wa jengo la ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) ambao unakadiriwa kugharimu shilingi Bilioni 1.6 mpaka utakapokamilika Machi 2025. Ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Magomeni.

Aidha, Kanali Sawala amekagua mradi wa maboresho ya Miundombinu ya usambazaji maji mijini Mtwara wenye jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 29.29 utakaojumuisha ujenzi wa matenki manne makubwa yenye uwezo wa kusambaza maji hadi lita laki sita kwa siku na uchimbaji wa visima viwili vikibwa.


Mradi mwingine uliotembelewa na Mkuu wa Mkoa ni wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani katika eneo la Mradi wa Samia City Mtaa wa Mjimwema ambao tayari umepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa awamu tatu tofauti.


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU 2025 KUPOKELEWA MKOANI MTWARA MEI 17

    May 15, 2025
  • MTWARA TUKO TAYARI KUUPOKEA NA KUUKIMBIZA MWENGE WA UHURU 2025

    May 14, 2025
  • UFUTA NA MBAAZI KUPIMWA KIDIGITALI MKULIMA KUPATA RISTI KUPITIA SIMU YAKE

    May 14, 2025
  • MKUU WA MKOA MHE. KANALI PATRICK SAWA AKAGUA MRADI WA MAENDELEO TANDAHIMBA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.