Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mtwara, Bi. Nanjiva Nzunda leo tarehe 14 Febfuari 2025 amezindua awamu ya kwanza ya mradi wa Uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti na tiba unaofadhiliwa na Wizara ya afya kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya JHPIEGO na Pfizer.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Bi. Nanjiva alieleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utazingatia malengo matatu makubwa ya Shirika la Afya la Dunia (WHO) ikiwa ni pamoja na Kuboresha huduma za uchunguzi wa kina kwa kuthibisha ugonjwa wa saratani ya matiti katika kipindi kisichozidi siku 60 tangu mteja kuonwa na mtoa huduma pamoja na kuhakikisha 80% ya wagonjwa waliothibitika na saratani ya matiti wanapata tiba stahiki.
Bi. Nanjiva aliongeza kwa kusema “Katika kuimarisha huduma za afya ngazi ya mkoa, kuna jumla ya vituo 45 venye uwezo wa kutoa huduma za kichunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti.”
“Saratani ya shingo ya kizazi na matiti ni tatizo kubwa, husababisha 10% ya vifo vya wanawake. Takwimu zinaonesha mkoa wa Mtwara tatizo ni kubwa zaidi kwani hakuna wadau wanaosapoti, sasa JHPIEGO wametuunga mkono ambapo tulianza mikoa ya Tanga na Mwanza na sasa tupo Mtwara na Morogoro.” Alieleza Dkt. Safina Lymo, mratibu kutoka Wizara ya afya.
Katika hatua nyingine, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara amezishukuru wizara ya afya pamoja na wizara ya fedha kwa kwa kuwaletea mradi huo pia amewasihi viongozi ngazi ya mkoa na halmashauri kuusimamia vema mradi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.