Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amewaambia wananchi wa Kata ya Nanguruwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kuwa Serikali imedhamiria kubadilisha maisha yao kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo sambamba na kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo alipopita katika Kata cha Nanguruwe na kuwasalimia wananchi kisha kutolea ufafanuzi juu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kutatua kero kubwa zinazowakabili wananchi wa hasa katika sekta ya maji na umeme.
Akitoa ufafanuzi wa tatizo la maji, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Primy Damas amesema kuwa Serikali imesaini mkataba wa sh. bilioni 5.7 wa kutoa maji Nanyamba hadi Nanguruwe ambao unatarajiwa kuanza kujengwa Julai, mwishoni na utakwenda kupunguza adha kubwa ya ukosefu wa maji katika maeneo ya kata hiyo na vijiji vilivyopo karibu nao.
Pia Mhandisi Damas amesema kuwa wameshachimba kisima kwenye hospitali ya Halmashauri iliyopo Nanguruwe na wanatarajia kufunga pampu ili wakabidhi kisima hicho ambacho kitakuwa na vizimba viwili nje ya hospitali ili visaidie kutoa maji kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.