Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema lengo la Serikali kutoa magari katika sekta za Elimu na Miundombinu ni kuimarisha ufuatiliaji wa ujifunzaji na ufundishaji katika shule za Mtwara sambamba na kuiongezea uwezo ofisi ya miundombinu kufuatilia utekelezaji wa miradi ya ujenzi inayoendelea ndani ya Mkoa wa Mtwara.
Kanali Abbas ameyasema hayo katika halfa ya kukabidhi magari matatu yatakayotumika kutoa huduma katika sekta za elimu na miundombinu huku akisisitiza kuwa hatua hiyo ni kielelezo Cha mkakati wa serikali ya Awamu ya Sita kuharakisha Maendeleo katika nyanja zote.
Aidha Kanali Abbas ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa jitihada kubwa inayofanya katika kuboresha sekta ya Elimu ikiwemo kuboresha miundombinu mbalimbali, kuongeza waalimu katika shule za msingi na sekondari, kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya uendeshaji wa shule sambamba na kununua vyombo vya usafiri kwa viongozi wa sekta ya elimu.
MWISHO.
“Mwezi Juni mwaka huu tumepokea walimu 157 wa shule za msingi na walimu 168 wa shule za sekondari ambao wamepokelewa na tayari wameanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali Mkoani kwetu” aliongeza Kanali Abbas.
Halikadhalika Kanali Abbas amesema kuwa pamoja na jitihada hizo, bado kuna changamoto ya upatikanaji wa chakula cha wanafunzi katika baadhi ya shule na hivyo kutoa wito kwa wazazi kuona umuhimu wa kuchangia huduma hiyo ili kuwawezesha watoto wao wapate chakula cha mchana wakiwa shuleni
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.