Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuhakikisha tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, Vituo vya Afya, Hospital za wilaya na mkoa nchini linakwisha kufikia mwezi Desemba mwaka huu.
Akijibu baadhi ya mabango yaliyowasilishwa kwake na wananchi wa mji wa Newala kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa Sabasaba Mjini Newala Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaboreshwa ili kuwaondolea wananchi kero ya upatikanaji wa huduma za afya. Aidha mpango huo unakwenda sambamba na mpango wa kuzipatia kila halmashauri, shilingi milion 500 za kujenga vituo vya afya kwa kila kata.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye yuko katika ziara ya siku tatu mkoani Mtwara amesema hadi kufikia mwezi wa 12 mwaka huu kila zahanati, kituo vya Afya na Hospitali za serikali zitakuwa na madawa ya kutosha hivyo kuondoa changamoto ya upungufu wa madawa. Pia amewaonya watendaji wa halmashauri, kutozichezea fedha hizo kwa matumizi mengine, kwa kuwa serikali haitavumilia kamwe vitendo hivyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.