Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewataka viongozi wa shule ya Sekondari ya wasichana Mtwara kuendelea kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundombinu ikiwemo Vyumba vya Madarasa na mabweni unaoendelea katika shule hiyo ili kufikia lengo la kusajili wanafunzi 472 muhula ujao.
Kanali Abbas ameyasema hayo mara baada ya zoezi la ukaguzi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo iliyogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 362. 2 na kusisitiza kuwa Serikali itahakikisha mtoto wa kike anapata haki yake ya kupata elimu katika mazingira bora na wezeshi.
Pia Kanali Abbas ametoa with kwa waalimu na walezi kusimamia kwa ukaribu suala zima la malezi ya wanafunzi wa kike ili kuwawezesha kutimiza malengo yao sambamba na maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetaka kuona mtoto wa kike anapata fursa ya kupata Elimu kama ilivyokusudiwa
Halikadhalika mara baada ya kujionea hatua ya ujenzi wa Miundombinu iliyofikiwa, Kanali Abbas alikabidhi zawadi ya boksi 51 za taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na chakula cha mchana hatua ambayo amesema inalenga kuwahamasisha kusoma kwa bidii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.