Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Wedson Sichalwe akipongezana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo wakati wakati hafla fupi ya kupokea magari ambayo yanalenga kuondoa changamoto ya utoaji wa huduma za afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepokea magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 na kusema kuwa magari hayo yataongeza thamani katika juhudi za serikali za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kabla ya kuyapokea magari hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) David Thompson katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ndogo za TAMISEMI zilizopo jijini Dar es salaam, Waziri Jafo alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya kusini.
Maelezo zaidi Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.